Viwanjani

Waziri Ummy Aipiga Tafu Klabu ya African Sports

on

 Katibu wa Klabu ya African Sports, Ismail Masoud katika aliyeshika funguo akizungumza mara baada ya
kupokea msaada huo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo ambao utakuwa chachu ya timu hiyo kumaliza ligi wanayoshiriki kwa ushindi.
 Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti
Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy
Mwalimu,Khatibu Kilenga aliyevaa kofia kushoto akiteta jambo na
viongozi wa klabu ya African Sports mara baada ya kukabidhi msaada huo
 Katibu wa Klabu ya African Sports Ismail Mosoud kulia akimshukuru Mwakilishi wa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM), Khatibu Kilenga kwa msaada waliotoa.


Mwakilishi wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na watoto Ummy Mwalimu, Khatibu Kilenga akiteta jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi salehe mara baada ta kukabidhi msaada huo.Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amekabidhi chakula na vifaa vyengine kwa ajili ya kuisaidia timu ya African Sports ya Jijini Tanga kujikimu katika kambi yao iliyopo maeneo ya Donge Tanga.

Msaada huo umefika wakati muafaka ambapo timu hiyo inajiandaa kuelekea michezo yao miwili iliyobakia ya ligi ya Taifa Daraja la Pili inayomalizika ndani ya wiki mbili.

Miongoni mwa vitu alivyokabidhi ni pamoja na Mchele kg 100,Unga wa ngano kg 50, Unga wa sembe kg 100, Maharage kg 50,sukari kg 50, mafuta ya kupikia lita 20,chumvi,sabuni na dawa za meno ambavyo vilikabidhiwa na Khatibu Kilenga kwa niaba ya Waziri Ummy.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kwa niaba ya Waziri Ummy, Kilenga aliwaambia wametakiwa heri katika michezo miwili iliyosalia kwenye michuano hiyo.

Aidha pia ni matumaini yake kwamba katika michezo hiyo timu hiyo itaweka bidii kubwa kuhakikisha inashinda .

Naye kwa upande wake, Katibu wa timu ya African Sports, Bw. Ismail Masoud alimshukuru Waziri Ummy kwa sapoti kubwa anayoionyesha na kwamba sasa wachezaji wamepata hari na nguvu ya kushinda mechi mbili zilizobakia.

Alisema mipango ya kushinda michezo hiyo iliyobakia ni mizuri ili kuhakikisha hawashuki daraja huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia timu hiyo kwani ni ya wananchi.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *