Viwanjani

Baada ya Kichapo Simba yamtimua Kocha Joseph Omog

on

Klabu ya Simba imeamua kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la FA wakiwa mabingwa watetezi.

Simba ilitolewa na timu ya Green Warriors inayoshiriki ligi daraja la pili katika hatua ya pili ya michuano hiyo kwa mikwaju ya penati 4-3 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo Hajji Manara inasema Uongozi pamoja na kocha huyo kwa pamoja wameamua kuvunja mkataba kwa mustakabali wa klabu.

Omog amekutana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wapenzi na mashabiki wa Simba ikichangiwa na usajili mkubwa uliofanyika msimu huu huku timu ikipata matokeo kwa bahati.

Kikosi cha Simba kitakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma mpaka atakapo patikana kocha mkuu.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *