Habari Kitaifa

Balozi Kidata Amuaga Makamu wa Rais Leo

on

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada, Balozi  Alphayo Kidata, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Kidata ambaye aliapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada tarehe 10, Mei 2018 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi  Kidata alifika leo kuona  Makamu wa  Rais  na kumuaga  rasmi  tayari kwa kwenda kulitumikia Taifa kwenye kituo chake kipya cha kazi nchini Canada.

Makamu wa Rais, Mhe. Samia amempongeza na kumtakia kazi njema ambapo alimtaka kwenda kufanya yale nchi imeelekeza haswa katika kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa Viwanda.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *