Uchumi Zone

Benki Kuu ya Tanzania yazifutia Leseni Benki tano Nchini

on

Gavana wa Benki  Kuu ya Tanzania anayemaliza muda wake Prof. Benno Ndulu amezifungia Benki tano pamoja na kusitishia shughuli zake zote za kibenki na kufuta leseni zake za biashara ya kibenki na kuziweka  chini ya ufilisi Benki hizo kutokana na  kushindwa  kufikia mtaji wa kiwango  kamili kinachohitajika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Prof. Ndulu amezitaja Benki hizo kuwa ni Covenant Bank for Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmer’s  Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited.

Prof. Ndulu amesema kuwa kutokana  na kutotimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mitaji kamili na wa kutosha, Benki Kuu kwa mujibu wa sheria za mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, imeamua kuzifungia na kusitisha shughuli zake zote za kibenki  na kufuta leseni zake za kibiashara ya kibenki.

Pia Prof. Ndulu amesema  kuwa Benki hizo zilipewa muda wa miaka mitano ili kuongeza  mtaji kufikia kiwango  kipya na muda huo uliisha mwezi juni 2017 na kuongezwa tena kwa kipindi  cha miezi sita hadi kufikia  tarehe 31 Desemba 2017.

Benki hizo hazikuweza kuongeza mtaji kufikia  kiwango kamili kilichohitajika pia zilishindwa kuandaa na kuwasilisha Benki Kuu  mpango mkakati unaokubalika  wa kuongeza mtaji na pia kuzifanya benki hizo kuwa endelevu na Benki Kuu pia imeiteua Bodi ya Bima ya Amana kuwa mfilisi wa benki hizo tano.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *