Viwanjani

Darlive waandaa Tamasha Usiku wa 900 itapendeza

on

Menejimenti ya Darlive kwa kushirikiana na Global group wameandaa tamasha maalumu ya kumtambulisha Dkt. Lous Shika kama miongoni mwa watu  waliopata umaarufu mkubwa kwa muda mfupi lakini pia kumpongeza kwa kushinda mnada wa nyumba za tajiri Lugumi na kumuweka rasmi kwenye muonekano mpya wa u bilionea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Meneja wa Dkt Shika Bi.  Catherine Kahabi amesema kuwa  lengo la tamasha hilo lijulikanalo kama “Usiku wa 900 itapendeza” linatarajiwa kufanyika rasmi usiku wa tarehe 9 desemba 2017 katika ukumbi wa Dar live Mbagala Zakheem na kuanza saa 11 jioni  na linatarajiwa kuhudhuliwa na  watu 5000.

Aidha Bi. Catherine ameongeza kuwa Mgeni rasmi wa tamasha  hilo ni  aliyekuwa Waziri wa  Mambo ya Ndani ya  Nchi Lawrence Masha ambaye  atafungua hafla hiyo, huku wakimtambulisha Mkurugenzi wa Global  Group Erick Shigongo kama mtu ambaye aliechangia kwa namna moja ama nyingine kujulikana kwa Dkt Shika.

Kwa  upande wake Dkt. Shika amesema kuwa  atazungumzia mambo mbalimbali ikiwemo historia  yake alipotoka na mpaka alipo sasa na kuahidi  kuelezea mengi kwa undani  zaidi hivyo  kuwaomba watu wajitokeze kwa  wingi katika usiku wa tamasha hilo.

Nae Meneja burudani wa Dar live Rajabu Mteta ameeleza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa  na burudani  mbalimbali ikiwemo Twanga  pepeta, Jahazi morden  taarab, wasanii  wa  bongo fleva pamoja  na wasanii wachekeshaji  kama vile  Mc  Pilipili, na  kuwasihi  wananchi mbalimbali kujitokeza kwa wingi usiku huo.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *