Habari Kitaifa

DAWASCO Yaadhimisha Wiki ya Maji Yaahidi Kushuhulikia Kero za Maji kwa Wananchi

on

Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam, (DAWASCO) limetakiwa kuhakikisha linashughulikia kero zote za maji kwa Wananchi ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na kupatia ufumbuzi tatizo la Maji Taka yanayotiririka holela kwenye makazi ya watu pamoja na upasukaji wa mabomba mitaani.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambapo amesema tatizo la maji taka limekuwa kero sugu katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo jambo linalohatarisha hata Afya za wananchi na kuwataka DAWASCO kuongeza jitihada za kufikisha huduma ya maji kwa wananchi ili kwenda na sera ya Serikali ya awamu ya Tano kwa kumtua mama ndoo kichwani.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisisitiza jambo wakati  akizungumza katika mkutano wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa mkoa huo na Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) jijini hapa.

Aidha Makonda ametoa wito kwa watumishi wa DAWASCO wanaokwenda kusoma mita majumbani kwa wananchi kuwa na kauli nzuri kwa wananchi kwani wao ndio wamekuwa wateja wazuri pamoja na kushughulikia kero za wananchi za kuwabambikizia kiwango kikubwa cha malipo ya bili za maji. 

Kuhusu changamoto ya upotevu wa maji na upasukaji wa mabomba Makonda amelitaka shirika hilo kulipatia majibu ya haraka tatizo hilo ili kiasi cha maji yanayopotea ili waweze kuwahudumia wananchi na kufikisha huduma ya maji kwa maeneo yenye changamoto na  uchimbaji  wa visima 50 vya maji ambapo amewasihi Wenyeviti wa mitaa hiyo kuainisha maeneo ya kuchimba visima hivyo.

 

Baadhi ya Watendaji wa Shilika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda (Hayupo pichani) wakati akizungumza na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Dawasco.

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam limepanga kutumia maadhimisho ya 30 ya Wiki ya Maji ilioanza leo kutoa elimu, kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati maalumu katika vituo vyote 10 vya DAWASCO vilivyopo katika jiji la Dar es salaam, Miji ya Kibaha na Bagamoyo  mkoani Pwani.

Utaratibu huo umelenga kutoa mwanga kwa wananchi wanaopata huduma ya maji Dawasco kupata elimu ya huduma ya maji na kusikilizwa kero na malalamiko yao ili kujenga ukarabati zaidi kati ya Dawasco na wananchi  na uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji umefanyika leo rasmi huku Kauli  mbiu ni “Hifadhi Maji na Mfumo wa Kikolojia kwa Maendeleo ya Jamii”.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *