Habari Kitaifa

DC Temeke Apiga Marufuku Askari Mgambo Kukamata Bodaboda katika Wilaya hiyo

on

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Felix Lyaniva amewataka madereva wa pikipiki na Bajaj kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama Barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu na viatu wakati wanapoendesha vyombo vya moto wakati wawapo barabarani ili kuepuka ajali zinazosababishwa na madereva wazembe na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo leo, wakati wa utambulishaji rasmi wa mfumo wa namba utakaowatambulisha madereva pikipiki na bajaj katika vituo vyao mbalimbali katika katika Kata ya Kibondemaji, Mbagala Jijini Dar es salaamu uliofadhiliwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Abdallah Said Mtinika kwa kushirikiana na Kampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaji Association (TAMOBA) kwa ajili ya kuzisajili Pikipiki na Bajaji katika mfumo wa GPS utakaowawezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza kupatikana kwa haraka zaidi.

Aidha Mhe. Lyaniva amewapiga marufuku mgambo wa wilaya hiyo kutokamata pikipiki na Bajaj kwani wengi wao wamekuwa wakikamata pikipiki hizo bila ya kujua na kuzingatia sheria na kuagiza kazi hiyo kufanywa na askari wenye weledi na wenye kujua sheria za usalama barabarani.

Mhe. Lyaniva pia amewapongeza TAMOBA kwa kuwafikia madereva bodaboda na bajaj kwani walikuwa na wasiwasi wa kuibiwa vyombo vyao na kuporwa na majambazi mbalimbali ila Diwani huyo ameleta maendeleo makubwa na mazuri katika Kata hiyo na pia TAMOBA imeleta usalama mzuri kabisa wa kisasa kwa kuwa madereva hao watafanya kazi zao wakiwa hawana wasiwasi wa kuibiwa Pikipiki zao na mali zao wawapo katika majukumu yao hayo pamoja na abiria wao.

Naye Diwani wa Kata ya Kibondemaji, Abdallah Said Mtinika amewashukuru TAMOBA kwani wameweza kumpatia refrector 300 kwa ajili ya madereva pikipiki katika kata yake hiyo na kuahidi kushirikiana na Bodaboda hao wa Kata yake.

Kwa upande wake, Afisa Utumishi wa TAMOBA Bw. Erasto Lahi amesema kwamba Kampuni hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2006 na lengo ni kuwalinda Madereva wa pikipiki na Bajaj na vyombo vyao hivyo vya moto na kuahidi kila bodaboda atapata sare ili kutambulika pia kuingizwa katika mfumo wa utambulishi utakaowatambua na kueleza mfumo huo utasaidia kuokoa gharama za kulipia Bima kubwa kwa kuwa kipengele cha hofu ya usalama wa chombo chake kitafanyiwa kazi masaa 24 labda iwe kwa sababu zingine, mfumo huu unawahakikishia wamiliki kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi watakuwa salama.

“Kila atakayesajiliwa na Kampuni hii atasajiliwa na mfumo maalum wa GPS utakaowezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo wapi, inatumiwa na nani na kuwezesha kui-lock hapohapo ilipoMtu aliye katika mfumo huu atapata msaada wa kulindwa kwenye mfumo muda wote masaa 24, hivyo mmiliki wa chombo muda wowote akihitaji taarifa za chombo kilipo, kilipopita na kinapoelekea atazipata, pia mfumo huu utaunganishwa na Jeshi la Polisi moja kwa moja ili kuharakisha zaidi huduma za kiusalama” alieleza Bw. Lahi.

Awali akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Katibu wa Bodaboda Kata hiyo ya Kibondemaji Bw. Hassan Habibu amemshukuru Diwani huyo ambae ni mlezi wao na  kueleza changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na baadhi ya askari shirikishi maarufu kama mgambo kuwakamata nyakati za usiku bila utaratibu wa kisheria na kuwapiga kwa kutumia magongo bila ya kujua makosa yao, pia kutopata mikataba ya uhakika kutoka kwa wamiliki wa pikipiki hizo wanazoziendesha.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *