Habari Kitaifa

Dkt KIGWANGALLA afunga Mafunzo ya 15 ya Jeshi USU

on

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wahifadhi wote nchini kushirikiana na wadau wengine hasa mamlaka za Mikoa na Wilaya katika maeneo yenye uvamizi wa mifugo na migogoro ya mipaka ya hifadhi ili kutatua changamoto hizo kwa namna shirikishi ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
 
Ametoa agizo hilo janaDisemba, 16, 2017 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa  TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.
 
“Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tutaiendeleza, Falsafa yetu ni kuwashirikisha wadau wote, kama kuna taasisi za kiraia kwenye eneo lako la kazi, taasisi za kijamii, mamlaka za mikoa na wilaya, wananchi, halmashauri husika mshirikiane nao ili kupunguza madhara ya operesheni zetu, na zoezi hili la uhifadhi liwe endelevu,” alisema Dk. Kigwangalla.
 
Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.
 
Awali akizungumzia mafunzo hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu, uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.
 
Tangu kuanzishwa kwa mafunzo hayo Septemba 2015 jumla wahifadhi 1468 wakiwemo Askari wa Wanyamapori na Viongozi mbalimbali kutoka TAWA, TANAPA na NGORONGORO wameshapatiwa mafunzo hayo katika kituo hicho cha Mlele.  
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) akikagua gwaride la Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimkabidhi cheti mmoja ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi Usu kati ya Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipokea salamu za Jeshi Usu wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiangalia onesho la kulenga shabaha liliofanywa na Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Dk. James Wakibara. 
Maonesho ya kulenga shabaha.
Maonesho ya kulenga shabaha.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *