Viwanjani

DKT. Kigwangalla Atoa Ofa ya Mapumziko ya Fungate ya Ali Kiba Katika Hifadhi za Wanyamapori

on

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dtk. Hamisi Kigwangalla ametoa ofa maalum kwa Mwanamuziki, Ally Kiba, mke wake na wasaidizi wake ambao ni mdogo wake Abdu Kiba na mkewe kupumzika katika Hifadhi ya Taifa atakayoichagua wakati wa fungate yake ili aweze kufurahi vivutio vya utalii vilivyopo na hivyo kuhamasisha utalii wa ndani. Ametoa ofa hiyo jana wakati wa harusi ya msanii huyo iliyofanyika katika ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa sherehe hiyo na Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Mgaya.

Picha ya pamoja katika sherehe hiyo iliyojumuisha Bwana Harusi, Ali Kiba, mke wake na wapambe wake na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimum, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na Mwenyekiti wa UVCCM Kheri James.

Picha ya pamoja ya maharusi na viongozi wa chama na Serikali pamoja na Gavana wa Jiji la Mombasa, Rashid Bedzima (wa pili kulia).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na  Wanamuziki, Ommy Dimpoz na Hamisi Mwanjuma Mwana  FA.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati wa sherehe hiyo.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *