Uchumi Zone

DKT. Mpango Akutana na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia

on

Mikutano ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2018 imeanza rasmi mjini Washington D.C. Katika mikutano hiyo kutakuwa na Magavana, Mawaziri wa Fedha, Sekta Binafsi pamoja na Wanataaluma mbalimbali kuweza kujadili  hali ya uchumi wa dunia pamoja na kupunguza umasikini.

Katika mikutano hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe, kuhusu maendeleo ya hali ya uchumi wa Tanzania huku akisisitiza kwamba ni wakati mzuri sasa wa kusemea hali ya uchumi wetu kwa nguvu zote.

Akiendelea kutoa ufafanuzi Dkt Mpango alieleza hatua ambazo Serikali imezifanya ili kuweka mazingira mazuri katika sekta binafsi, na kwamba Serikali imeandaa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika Taifa la Tanzania.

Pia Waziri Mpango alielezea miradi mikubwa ambayo nchi imeanza kuitekeleza, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa na Ujenzi wa Bwawa  kubwa la kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la ‘Steigler’s Gorge’ katika Maporomoko ya Maji ya MtoRufiji.

Kupitia miradi hiyo ambayo Serikali imepanga kuifanikisha kwa wakati Dkt. Mpango alimuomba Bw. Bvumbe kuendelea kuzungumza na uongozi wa Benki ya Dunia ili uweze kutusaidia katika kuwezesha uwekeza katika miradi hiyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa jitihada inazozionesha hasa katika kupambana na rushwa na ametutia moyo tuendelee na juhudi zetu za kuimarisha uchumi wetu hususani katika sekta ya kilimo na pia amefurahishwa na hatua mbalimbali zinazofanya kwa ajili ya kuendeleza sekta ya viwanda.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *