Habari Kitaifa

Dkt MPOKI ULISUBISYA: Wauguzi ni chachu ya huduma Bora nchini

on

Wauguzi wakuu wa Mikoa na hospitali za Taifa na Rufaa za Kanda wametakiwa kusimamia maadili ili kupunguza malalamiko toka kwa wananchi

Hayo yamesemwa  jana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya wakati wa mafunzo juu ya maadili kwa wauguzi wakuu yanayoendelea mjini hapa kwenye chuo cha uuguzi na ukunga Mirembe

Dkt.Mpoki alisema  hivi sasa kumekua na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya huduma wanazozitoa hivyo kupitia mafunzo hayo wanapaswa kusimamia ipasavyo maarifa na mikakati watakayojiwekea ili kuleta mabadiliko makubwa na kuondoka malalamiko hayo.

“Jamii na Serikali inawategemea sana katika usimamizi wa huduma bora nchini,naamini kwamba ninyi mna nguvu,nia na maarifa katika kuboresha maadili ya wauguzi wote nchini,hivyo ni muhimu mkasimamie”alisema Dkt.Mpoki

Aidha, alisema wizara yake inatambua umuhimu wa kuboresha maadili hususani kwa wauguzi,hivyo kuwapatia mafunzo kama ni muhimu kwa taaluma yao.

“Kumekuwepo na malalamiko na ongezeko kubwa la vitendo visivyo vya kiadilifu kwa watumishi wa afya ikiwa ni pamoja na kauli mbovu kwa wagonjwa,naamini kwa mafunzo haya changamoto zote mtazijadili na kusaidia kuondokana na malalamiko toka kwa Wananchi”

Naye Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga wizara ya afya Gustav Moyo alisema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa namna gani ya kuboresha uadilifu na maadili ya sehemu zao za kazi wauguzi nchini

Aidha,ametoa wito kwa wauguzi wote nchi kuzingatia Iadilifu,utu,upendo na maadili yao ya kwa kuipatia thamani stahiki taaluma yao kwani wauguzi ndio wanaokuwepo muda wote mahali pa kazi

“Serikali ya awamu ya tano inasisitiza suala la uadilifu hivyo wananchi wanahimizwa kuwabaini na kuwasema ili kuwabaini baadhi ya  wanaokiuka maadaili au kufanya vitendo visivyozingatia maadili ili tuwachukulie hatua ama kurekebisha na tuweze kutoa huduma yenye viwango na inayokubalika na salama kwa wananchi”.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *