Viwanjani

DKT. Mwakyembe aahidi kusaidia Wanafunzi wanaosoma Multi Media

on

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeahidi kuwasaidia wanafunzi wanasoma kozi ya Multi Media kupata nafasi za mafunzo kwa vitendo katika sehemu mbalimbali pale inapowawia vigumu kupata nafasi hizo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alipotembelea Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa lengo la kufahamu  kozi ya Multi Media inayotolewa na chuo hicho namna gani inaweza kusaidia  uandaaji wa filamu nchini.

“Kozi hii ya Multi Media ni moja ya masomo yanaweza kuisaidia sekta ya filamu kupata taswira mpya tofauti na ilivyosasa kwani wataalamu hawa wakitumiwa vizuri katika kuandaa filamu  za hapa nchini wanaweza kuleta mabadiliko kwani kwa sasa sekta hiyo ina changamoto kubwa ya kukosa waandaji wenye weledi.” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe aliwapongeza wanafunzi wa chuo hicho kwa kuonyesha weledi pale walipokuwa wakijibu  maswali waliyoulizwa  kuhusiana na namna wanaweza kuboresha uandaaji wa filamu ambapo wanafunzi watatu tofauti walijibu kwa ufasaha.

Naye Katibu wa Bodi ya Filamu Nchini Bi. Joyce Fissoo alipongeza uongozi wa chuo hicho na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na taasisi hiyo kwa lengo kwa kuwashauri waandaaji wa filamu nchini maarufu kama bongo movie kwenda kusoma katika chuo hicho lengo la kujiongezea weledi katika kazi yao.

“Kuna changamoto kubwa kwa waandaaji wa filamu nchini na tumekuwa tukiwaeleza hilo mara kwa mara lakini shida kubwa ni kwa baadhi yao kukosa wa elimu ya kutosha hivyo tutaendelea kutoa msisitizo wa waandaji hao kuhakikisha wafanya kozi mbalimbali za uandaaji wa filamu kwa lengo la kujijengea weledi katika kazi yao” alieleza Bi. Fissoo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Teknolojia (DIT) Prof. Preksedis Ndomba alieleza kuwa kozi hiyo ya Multi Media kwa mwaka juzi ilikuwa na wahitimu kumi na mbili wa Stashahada na kumi kati yao tayari wameshapata ajira katika sehemu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kwenye vyombo vya habari na kwa mwakani kuna mpango wa kuanzisha shahada.

Prof. Ndomba alieleza Darasa hilo la Multi Media limekuwa na changamoto ya rasilimali mbalimbali kama vifaa vya kurekodia wakati wa vipindi sababu darasa hili ni huitwa (smart class) hivyo uendeshaji wa vipindi vyake hutegemea zaidi mtandao.

Halikadhalika Mmoja wa wanafuzi wa Chuo hicho anayesomea Stashahada ya Multi Media Agatha John alieleza kuwa kuputia chuo hicho amepata uelewa mkubwa wanamna ya kuandaa filamu na vipindi kwa vyombo vya habari hivyo anaamini anaweza kufanya kazi hiyo kwa kujiamini na weledi.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *