Habari Kitaifa

Dkt NDUGULILE ashiriki Ujenzi wa Shule Wilayani Kisarawe

on

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile ameshiriki kazi ya ujenzi wa shule ya msingi Chambasi Wilayani Kisarawe ikiwa ni zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Dk. Ndugulile amesema kuwa kwa kipindi kirefu dhana ya wananchi kujitolea katika kufanya kazi za maendeleo imepungua kwa kiasi kikubwa na kuiachia Serikali ikitoa kila kitu kutekeleza miradi ya maendeleo hata kama inawezekana kazi hizo kutekelezwa na wananchi.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa kwa kipindi cha sasa cha Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa kazi tu wananchi hawana budi kujitoa katika kufanya shughuli za maendeleo katika maeneno hayo ili kuisaidia Serikali na kujisaidia wao wenyewe kujiletea maendeleo.

“Msisubiri kila kitu kifanywe na Serikali vingine mnaweza kufanya weneyewe hongereni sana ninyi ni mfano wa kuigwa kwa vijiji vingine katika hili” alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chambasi Bi. Fodia Makebu Tungaraza amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa shule umeibuliwa na wananchi wenyewe mara baada ya watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda kijiji cha jirani kuifata shule ya Msingi Msimbu takribani kilomita sita hivyo kuhatarisha maisha na usalama wa wanafunzi hao.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msimbu Bw. Hussein Mkambara  ambae pia anayesimamia shule ya Chambasi hadi itakapopata usajili ameishukuru Serikali kwa kuona na kuwaunga mkono katika jiitihada za kujikwamua katika changamoto waliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile amefanya ziara ya siku moja mkoani Pwani wilaya ya Kisarawe kwa kushiriki ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Chambasi, kuvitembelea vikundi vya wanawake vinavyojishughulisha na biashara na viwanda vidogo vidogo vinaowezeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na kutembelea Mahakama inayohusika na mashauri ya watoto wilayani Kisarawe.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *