Habari Kitaifa

Dkt. Ndugulile avitaka Vyombo vya Usalama kuimarisha mifumo ya kudhibiti upotevu wa dawa Kigoma

on

Serikali imeviagiza vyombo vya usalama na kamati za Afya za vijiji kuimarisha mifumo yote ya udhibiti wa upotevu wa Dawa nchini, kwa kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, ili kuondoa ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ziara yake katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma ya kukagua utoaji huduma za Afya na kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya jamii ambao unasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi.
“Niwaombe sana ndugu zangu wananchi tuwe walinzi, hiyo dawa ingeweza kukusaidia wewe, au ndugu yako, hivyo kushiriki katika ubadhilifu huo ni kujiumiza mwenyewe.” alisema Dkt. Ndugulile.
Katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto Dkt. Faustine amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewekeza kiasi cha shilingi Milioni 400 katika Halmashauri 175, kikiwemo kituo cha Afya cha Uvinza , fedha zitakazotumika kuboresha na kujenga vyumba vya kutolea huduma ya dharura wakati wa kujifungua, nyumba za watumishi pamoja na maabara.
Dkt. Ndugulile amesema kwamba, Serikali inaendelea kufanya vizuri barani Afrika na Dunia kwa ujumla kwa upande wa utoaji chanjo, kwani imefikia asilimia 97 ya walengwa  wote wanaohitaji chanjo nchini jambo linalosaidia kutunza Afya za watu katika jamii.
Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa anatambua uhaba wa watumishi unaovikabili vituo vingi vya Afya katika Wilaya ya Uvinza ambao umefikia asilimia 66 na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo ili kupunguza  changamoto katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza Bajeti ya dawa , kutoka Bilioni 30 mpaka Bilioni 270 wa mwaka huu wa fedha hali iliyosaidia kuimarisha mapambano dhidi ya maradhi mbali mbali.
Aidha, Dkt. Ndugulile aliwapongeza wananchi wa kata ya Kazuramimba kwa kuonesha kwa vitendo utayari wao wa kusukuma guruduma la maendeleo ya elimu katika Kijiji hicho kwa kuamua kujenga madarasa ya shule katika Kijiji cha Nyanganga kilicha kata ya Kazuramimba ili kuweza kuwakomboa watoto wao na janga la ujinga na umasikini.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi Mwanamvua Mlindoko ameeleza faida ya mradi wa ujenzi wa madarasa ikiwemo ongezeko la ufaulu kutoka wanafunzi 4115  mwaka 2017 huku waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi 1641 ambao ni sawa na asilimia 36 tu, hivyo kutokana na ujenzi wa madarasa haya utasaidia wanafunzi 2482 sawa na asilimia 64 kuendelea na elimu.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *