Habari Kitaifa

DKT. Ndungulile: Watu milioni 7 Wanakadiriwa kuwa na Shinikizo la Macho “Glaucoma”

on

Serikali imesema kuwa inakadiriwa watu takribani  milioni 253 duniani wenye matatizo ya kutokuona vizuri kati yao milioni 36 hawaoni kabisa na zaidi ya asilimia 75 ya visababishi vya kutokuona  vizuri vinaweza kuzuilika ama kutibika na  asilimia  2.8 ya watu wote  wenye upungufu wa kutokuona vizuri sawa  na watu milioni 7 duniani wana ugonjwa wa shinikizo la Jicho kati yao  milioni 4.5 hawaoni kabisa.

Akizungumza leo jijini Dar es  salaam, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee  na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Takwimu za Shirika la Afya duniani zinakadiria kuwa ifikapo mwaka 2020 idadi ya watu wasioona kutokana na ugonjwa wa shinikizo la Macho itafikia milioni 11.2 ongezeko hili ni kubwa na kunahitajika jitihada zaidi katika kuwatambua watu  wote wenye tatizo ili na kuwapatia matibabu mapema kabla uwezo wao wa kuona haujapotea.

Aidha ameongeza kwa Afrika ugonjwa wa Shinikizo la Jicho unachangia asilimia 15 ya watu wasiona, na ugonjwa wa shinikizo la macho unaathiri zaidi watu wenye umri  wa miaka 40 na zaidi na  kwa Tanzania inakadiriwa kuwa  asilimia 4.2 ya  watu wenye umri  zaidi ya miaka 40 wana  ugonjwa huu sawa na watu 440,000 na isivyo bahati asilimia 70 hadi 90 ya watu wenye  ugonjwa huu hawajijui iwapo wanao ugonjwa huu, Hii inatokana na kuwa wengi wao hawana tabia ya kuchunguza Afya ya Macho kama inavyoshauriwa na wataalamu.

Kulingana na  Takwimu za Shirika la Afya Duniani, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 1,740,000 wana matatizo ya kutokuona vizuri kunakosababishwa na matatizo yote,  matatizo yanayoongeza  Mtoto wa Jicho tatizo la upeo mdogo wa macho kuona ikifuatiwa na shinikizo la macho na  kwa mwaka  2017, ni  watu 13,240 tu waliohudhuria kwenye vituo vyetu vya tiba wakiwa na tatizo la shinikizo la macho idadi hii  ni ndogo ikilinganishwa na watu walio kwenye hatari ya  kuwa na  ugonjwa huu ambao wapo kwenye jamii yetu hawajagunduliwa.

Maadhimisho ya wiki ya elimu ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho huadhimishwa duniani kote ikiwa ni mpango ulioanzishwa na Chama cha Wagonjwa wa Shinikizo la Macho na Chama cha Wataalamu wa Afya wa Shinikizo la Jicho kwa lengo kuu la kuongeza uelewa na kujenga ufahamu wa wananchi juu ya ugonjwa huo hatari ujulikanao kwa kitaalamu kama “Glaucoma” au Presha ya Macho katika  azma ya  kuzuia ulemavu wa kutokuona na  Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha wiki hii muhimu ya Afya ya Macho, na  maadhimisho hayo yanafanyika wiki ya tarehe 11  mpaka 17 mwezi machi.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *