Viwanjani

HARMONIZE ajumuika pamoja na Watoto yatima Kupata Chakula

on

Msanii wa muziki wakizazi kipya Rajab Abdulkahal au Harmonize amekula chakula cha mchana na watoto wanaishi katika mazingira hatarishi katika kituo cha kulelea Yatima cha kanisa LA EAGT mkoni Mtwara kama moja ya Kuwapa matumaini katika Maisha ya kila Siku.

Harmonize akiongozana na rafiki yake wa kike wa karibu Anayejulikana kwa Jina la Sarah amesema kuna watoto waliopoteza wazazi wao wakiwa na umri mdogo huku wakiwa na ndoto kubwa za kimaisha lakini zinaonekana kupotea kutokana hivyo wanahitaji kupewa moya na kuwa na bidii binafsi.

Hata Hivyo Msanii Harmonize amepata fursa ya kubadilishana Mawazo na watoto wenye Ndoto mbalimbali zankimisha na kuwasihi kumshirikisha Mungu kwa kila wanachokifanya.

Harmonize akiongea na Wandishi wa Habari Mara baada ya kumaliza Chakula cha Mchana alichokiandaa kwa ajili ya Watoto Yatima Mtwara.

Msanii Harmonize akiwa na Rafiki yake Sarah wakigawa chakula kwa Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi ambao wanalelewa katika kituo cha Kulea Yatima cha EAGT Mtwara.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *