Habari Kitaifa

Wizara Yajipanga Kuimarisha Utendaji Kazi

on

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii) imetakiwa kujipanga kimakakati ili kufanikisha malengo ya utendaji wake ili kuleta matokea chanja katika jamii.

Hayo yamesemwa na waendesha Mafunzo kwa ajili ya kuimarisha utendaji na kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi, weledi na uadilifu katika Wizara yanayofanyika mjini Dodoma.

Mmoja ya watoa mada katika mafunzo hayo  Bw. Alphonce Muro amesisitiza kuzingatia Kanuni ya utatu  yaani Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa ndani katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuhakiki, kusimamia na kudhibiti utendaji mahali pa kazi ili kuongeza thamani ya huduma na kazi za kila upande katika kufanikisha malengo ya Wizara.

“Uhusiano na mawasiliano kati ya watendaji hawa ni muhimu katika kufanikisha maelengo ya Wizara” alisema Bw. Muro. 

Naye mtoa mada  kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, katika Ofisi ya Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bw. Athanas Pius  amesema kuwa kila upande una wajibu wa msingi katika kuchangia kufikiwa kwa malengo ya Wizara kwa kuwa na mawasiliano na kushirikiana katika kupokea na kutekeleza ushauri wa kitaalam unaotolewa na maafisa wa Kitengo cha Ukaguzi na Kamati ya Ukaguzi wa Ndani kwa lengo la kuboresha utendaji na usimamizi.

Akiwasilisha mada ya Majukumu ya Kamati ya Ukaguzi ya Wizara, Bw. Athanas Pius amebainisha kuwa maafisa wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara wanawajibu wa kutoa ufafanuzi wa masuala ya kitaalam ambayo yatashirikisha wataalam wa fani mbalimbali katika uhakiki na uandishi wa taarifa husika.

 “Ushauri huu wa kitaalam kimsingi unahitaji utekekezaji ili kuongeza thamani katika utendaji, usimamizi na uadilifu mahala pa kazi” alisema Bw. Pius

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi Bw. January Katunzi, amebainisha kuwa mafunzo yamewajengea uelewa wa kuweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, kuaminiana na kuwasilianaili kongeza thamani ya ubora wa huduma za Wizara.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Menejimenti kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii  Bi.Silivia Siriwa amepongeza wawezeshaji wa mafunzo hayo kwa elimu waliyotoa ambayo itawasaidia kuboresha mifumo ya utendaji kazi ndani ya Wizara na Taasisi zake ili kudumisha uadilifu, utawara bora na ufanisi kazini.

Akizungumza kwa niaba ya wataalam wa Kitengo cha Ukaguzi cha Wizara Bw. Dickson ameongeza kuwa uzingatiaji wa utendaji unaoongeza thamani na ubora kazini utafikiwa kwa kuwa na watumishi waadilifu, mifumo sahihi na uwajibikaji wa pamoja.

Mafunzo hayo siku mbili yanaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma yamejumuisha wajumbe wa Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa Ndani ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii).

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *