Habari Kitaifa

IFM na Tehama kwa Tanzania ya Viwanda

on

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimefanya kongamano la masuala ya teknolojia na mawasiliano Jijini Dar es Salaam ambapo lengo la kongamano hilo ni kuwajenga wanafunzi, kuzalisha wataalamu juu ya masuala ya teknohama ili kuendana na Serikali ya viwanda kwa kupata wataalamu wengi.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kongamano hilo Mkufunzi Mkuu wa masuala ya Teknolojia ya mawasiliano na mahesabu kutoka( IFM) Dkt. Eliamani Sedoyeka amesema jukumu la kongamano ni kueleza na kuonyesha umuhimu wa masuala ya teknolojia katika nyakati hizi ili kuweza kupata watu bora wa kuweza kushindana katika soko la ajira Nchi za Afrika Mashariki ambapo kongamano hilo likiwa ni la tatu kufanyika na kuwa na muitikio mkubwa wa watu mbalimbali kutoka sehemu nyingi.

“Kongamano hili limeweza kuleta watu mbalimbali wa masuala ya ICT na sio kutoka IFM tu bali kutoka vyuo vya CBE, UDSM, NA TIA, pia limeleta wawakilishi wengi kutoka Nchi za nje kama Afrika Kusini, Kenya, Botswana na hapa kwetu Tanzania” Alisema Dkt. Sedoyeka.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tehama kutoka IFM Dkt. Deniss Lubiana ameeleza kuwa chuo chochote kile lazima kiwe kinafanya utafiti ili kutoa takwimu sahihi hvyo kongamano limefanikiwa kupata tafiti 10 ambazo kama wadau wakubwa wa masuala ya teknolojia wanajivunia kwa hatua kubwa hiyo walioifikia.

Pia Dkt. Lubiana amesema kongamano hilo limefanikiwa kutokana na michango ya masuala ya IT na kujifunza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na kutoa shukrani zake za dhati kwa wote waliofika kufanikisha kongamano hilo.

About Filbert Yudatade

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *