Habari Kitaifa

Jiji la Dar es Salaam lapata tuzo Kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka

on

Jiji la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017  kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Katika tuzo hiyo  mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka huu.

Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo  na Jiji la New York  nchini Marekani na Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.

Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *