Uchumi Zone

Kampuni ya Kilimanjaro SAR LTD Yaingia Makubaliano na Hospitali ya St. Joseph

on

Sekta ya Utalii nchini imepata suluhu ya Changamoto ya muda mrefu ya utoaji wa msaada wa kitabibu, utafutaji na uokoaji wa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru .

Changamoto hiyo inafika kikomo rasmi baada ya kampuni ya Kilimanjaro SAR kuzindua Kliniki ya kwanza Afrika ya magonjwa yatokanayo na muinuko wa juu pamoja na utumiaji wa Helkopta kwa ajili ya uokoaji katika Hifadhi za Mlima Kilimanjarona Mlima Meru.

Mbali na uzinduzi huo Kilimanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi ,kuanza kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa watakao pata matatizo wakati wa kupanda Milima hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano kati ya Kampuni ya Kilimanjaro SAR na Hospitali ya St Joseph ,Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba aliyekuwa mgeni rasmi amesema hii ni fursa mpya kwa sekta ya Utalii kuutangaza vyema Mlima Kilimanjaro.

Huduma hii ya kwanza kutolewa barani Afrika inaiweka Tanzania katika nafasi ya pili katika Ramani ya Dunia, kuwa  na kliniki ya kipekee katika utoaji wa huduma kwa wapanda Mlima na kwamba kwa kiasi kikubwa itasaidia katika kuongeza idadi ya Watalii. 

Hata hivyo kuanza kwa huduma hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini ,bado ipo changamoto ya matumizi ya uwanja mdogo wa ndege wa Moshi hali inayowalazimu kutumia uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Ulbanie Lyimo ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph akaeleza faida itakayopatikana kutokana na kuingia makubaliano na kampuni hiyo ya Uokoaji ya Kilimanjaro SAR kuongeza maarifa katika utoaji wa matibabu kutoka kwa madaktari wa kigeni watakao hudumia wagonjwa wa Mlimani.

Kuanza kwa kliniki hii ni msaada kwa maiha ya wapandaji wa Mlima Kilimanjaro na Meru ikizingatiwa asilimia 75 ya magonjwa uwapo mlimani yanatokana na mbadiliko ya Hali ya Hewa kulingana na urefu wa Mlima.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *