Habari Kitaifa

Kandege Apongeza Usimamizi wa Ujenzi wa Vituo vya Afya Arusha

on

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amepongeza usimamizi mzuri uliofanyika katika ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Jijini Arusha.

Mhe. Kandege amesema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara hivi karibuni ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Nduruma kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Jiji la Arusha na Kituo cha afya cha Usa River Kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Jijini Arusha.

Aidha amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya Jijini Arusha, na kuwapongeza kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo ni imara na yanaendana na dhamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

“Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya katika Jiji la Arusha ipo vizuri na kazi inayofanyika inaridhisha ukilinganishwa na fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini.

Mhe. Kandege ametoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha miradi inakamilika kwa  wakati ili huduma za afya ziweze kutolewa kwa wananchi.

Amezitaka Halmashauri kutengeneza mazingira mazuri ya vituo vya afya nchini ikiwa ni pamoja na kuweka uzio, kupanda miti hasa ya matunda ili kutengeneza mandhari inayovutia kwa wagonjwa pindi wanapohitaji kuaptiwa huduma ya afya.

Akiongelea kuhusu vyumba vya kujifungulia wanawake wajawazito Mhe. Kandege ameelekeza chumba cha kujifungulia kitenganishwe kila kitanda ili kuwa na usiri wa mama mjamzito anapojifungua.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *