Habari Kitaifa

Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme Gongolamboto Chawashwa

on

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Gongolamboto chenye uwezo wa MVA 65 na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mgalu alisema Kituo hicho  kinapokea umeme  kutoka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi katika line ya 132 kV.

Mgalu alifafanua kuwa kukamilika kwa kituo hicho kumewezesha uboreshaji wa upatikanaji wa umeme  katika maeneo ya Kurasini, Kipawa, Kitunda, Chanika na Kisarawe,  Ubungo, Mbagala na GongolaMboto.

“Kwa sasa hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yaliyokuwa yakisambaziwa umeme kutoka katika kituo hiki haitakuwepo tena, hivyo Serikali itaendelea na juhudi kuwasha umeme katika vituo vingine vilivyosalia,” alisisitiza Mgalu.

Kituo cha Gongolamboto ni miongoni mwa vituo 19 vya kupoza na kusambaza umeme nchini vilivyo katika mradi wa uboreshaji wa vituo hivyo unaofadhiliwa na TEDAP  ambapo Jiji la Dar es salaam lina vituo 11,  Arusha vituo Sita (6) na Kilimanjaro vituo viwili (2).

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akipata maelezo ya uendeshaji wa kituo cha Gongolamboto , kutoka kwa  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James,(mbele)  wakati akikagua mitambo ya kituo hicho kabla ya kuwasha kwa mtambo huo.kushoto ni Kaimu Meneja Miradi , Mhandisi Emmanuel Manirabona.

Baadhi ya watendaji katika kituo cha Gongolamboto, wakikamilisha kazi kabla ya kuwasha umeme katika  kituo hicho.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wapili kushoto) akizungumza na mkandarasi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala. kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James.

Transfoma iliyofungwa mwaka 57, ( kulia) iliyokuwa ikifanya kazi ya kusambaza umeme katika kituo cha Gongolamboto,na mpya zilizowekwa sasa (kushoto).

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *