Viwanjani

TBC, Kwese Free Sports (TV1) Kurusha Michuano ya Kombe la Dunia kwa Kiswahili

on

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Kwese Free Sports  wameingia makubaliano ya mkataba wa ushirikiano kwa ajili kurusha matangazo ya michuano ya fainali ya Kombe la Dunia kwa lugha adhimu ya kiswahili yanayotarajiwa kuanza tarehe 14 mwezi wa sita hadi 14 mwezi wa saba.

Kwa kupitia ushirikiano huo mahususi wa KFS Tanzania na televisheni ya Taifa TBC , watanzania wanapewa nafasi ya kuungana na mabilioni ya watazamaji kutoka kote duniani kushuhudia michuano hii pasipo kuingia gharama yoyote ukiwa ni mbadala nafuu kwa mtanzania mwenye kipato cha kawaida.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika hafla hiyo Mkurugenzi KFS Tanzania Bw. Joseph Sayi amesema michezo ni moja kati ya maeneo muhimu katika tasnia ya burudani  nchini  Tanzania  na duniani kote na kwa sababu hiyo KFS Tanzania inajivunia kuwapa fursa ya kutazama moja kwa moja mashindano makubwa ya kimichezo duniani.

“Tunashukuru sana wenzetu wa TBC kwa kutupa ushirikiano huu kudhihirisha hili lengo letu ni kutoa kipaumbele katika michezo naburudani kwa watazamaji wetu, tunawaletea  michezo ya Kombe la Dunia moja kwa moja mpaka majumbani mwao bila ya gharama yoyote, FIFA World Cup ni michuano inayotazamwa na watu  wengi kuliko yote duniani ikiwa na washabiki wapatao billioni 3” amesema Bw. Sayi.

Naye Mkurugenzi wa Masoko TBC  Daphrosa Kimbory amesema kuwa wanafurahi kwa hatua kubwa waliyoifikia kama kituo na jukumu lao ni kuona watanzania wanapata fursa ya kushuhudia matangazo hayo ya fainali za kombe la dunia bure bila malipo yoyote na michuano hiyo itakuwa ikirushwa kupitia TBC 1, TBC Taifa pamoja na TV 1.

“Tunatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na KFS Tanzania tukiunganisha mamilioni ta watanzania watakaokuwa wakitazama michuano hii katika kituo chetu bila ya malipo yoyote na tunawafikia walengwa wengi zaidi kupata fursa hii ambayo na amini watanzania wataipokea na kuifurahia” amesema Bi. Kimbory.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa KFS Tanzania Gillian Rugumamu amesema kwamba KFS ni channel ya bure ya michezo pekee nchini na imejitengenezea wasifu kwa kuzalisha na kurusha vipindi bora zaidi kuanzia vipindi vya hapa nyumbani, vya barani Afrika hadi kimataifa vinavyoendana na watazamaji wake.

Aidha Bw. Rugumamu ameongeza kuwa ni jambo la furaha  kwao kuleta Kombe la dunia kwa watanzania hususani washabiki ikiwa ni nyenzo ya kukuza na kuimarisha uhusiano wao na watazamaji hususani mashabiki wa michuano hiyo ya mchezo huo mpira wa miguu.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *