Habari Kitaifa

Makamu wa Rais afungua Soko la Konde-Pemba

on

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi inatekeleza sera mbali mbali zenye muelekeo wa kupunguza umasikini.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Soko jipya la kisasa lililopo Konde, Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Makamu wa Rais alisema Sekta ya kilimo inatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 70 na inachangia kiasi cha asilimia 50 ya chakula kinacholiwa Zanzibar, hivyo ni jukumu la Serikali kuweka mazingira bora kwa wananchi ili waweze kujiletea maendeleo.

“Soko hili la kisasa litapelekea kuongezeka kwa ajira, kupitia kuongezeka kwa shughuli za kibiashara na kilimo, kuongezeka kwa uzalishaji, na uongezaji thamani wa mazao, hata kuongezeka kipato cha mtu mmoja mmoja  na Taifa kwa ujumla”.

Makamu wa Rais alisema ni dhahiri kwamba kuondoka na umasikini kutategemea sana mafanikio ya shughuli zinazotekelezwa katika sekta ya kilimo  “hivyo ni vyema tukaboresha kilimo kwa kubuni fursa zaidi na kuongeza kipato kwa wananchi wetu”.

Makamu wa Rais alitoa wito kwa uongozi wa Shehia, halmashauri, Wilaya na mkoa kuhakikisha kuwa soko linasimamiwa kwa ukaribu na linatumiwa kwa kuzingatia taratibu zitakazohakikisha uendelevu wa huduma zitakazotolewa na kuona malengo yaliokusudiwa yanafanikiwa ikiwamo kuwaletea wananchi mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.

Aidha Mama Samia aliwataka wananchi kuendelea kuwa kitu kimoja katika kulienzi soko ili liweze kuboresha maisha yao nay a vizazi vijavyo

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema  kuwa maendeleo yanayojengwa leo ni mmoja ya azma kubwa ya Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyesema kuwa “Tunataka kuweka hali za wananchi sawa” na ndio maana Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amejitahidi kuleta maendeleo sawa sawa kila pahala.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *