Habari Kitaifa

Makamu wa Rais awaasa Viongozi wa Dini kuhubiri Amani na Usalama

on

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Dini nchini kuunga mkono azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora.

Makamu wa Rais amesema hivi karibuni Serikali imepitisha mabadiliko na mpango mpya wa uwekezaji Tanzania.

Makamu wa Rais amesema kuwa kudumisha Amani na usalama ni jukumu la wote “Endeleeni  kuhubiri Amani na kwa upande wa Serikali ni wahakikishie Watanzania wote kwamba Amani na Usalama ni kipaumbele chetu hatutavumilia kumstahimilia mtu yeyote yule ambaye ana lengo la kuharibu Amani ya Tanzania hatutamvumilia tutamshughulikia ipasavyo”

Makamu wa Rais amesema “Tukosoeni pale tunapokosea nasi tunawaahidi tutarekebisha na twende mbele kwani Mwalimu Nyerere alituambia kuongoza ni kuonyesha njia na katika kuonyesha njia lazima ukubali kukosolewa nasi tunakubali kukosolewa hilo nalo ni jukumu la utumishi wa kiroho kwa hiyo endeleeni kutukosoa kwa ile lugha ambayo tutafahamiana”.

Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Taasisi za dini katika masuala ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii.

Makamu wa Rais amelishukuru na kulipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa mchango wake mkubwa unatoa katika nchi yetu hususani katika Nyanja za Elimu, Huduma za Afya naMaji.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Fredrick Shoo alisema kuwa wameona jitihada za Mheshimiwa Rais na wataendelea kumuunga mkono  na wapo pamoja kushirikiana na Serikali kwa nia njema kabisa.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *