Habari Kitaifa

Makamu wa Rais awahimiza Wananchi kuwa na Bima ya Afya

on

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ufumbuzi umepatikana wa changamoto kubwa ya umeme inayoikabili hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila na kuahidi kusimamia utendaji ili umeme upatikane muda wote.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba, na kusema kwa vifaa vya kisasa vya umeme vilivyopo hospitalini hapo havipaswi kupata umeme wa mashaka.

Makamu wa Rais amesema kuwa  wananchi wengi hawajajua umuhimu  wa kuwa na bima  ya afya hivyo  elimu zaidi  itolewe ili wananchi wengi wachangie huduma ya afya kwa kupitia bima zao hii itawapunguzia gharama sana wakati wa matibabu.

Makamu wa Rais aliutaka  uongozi wa Mloganzila kutangaza kwa wananchi huduma zinazopatikana hospitalini hapo ambapo wana vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi wa afya, Makamu wa Rais alisema huduma ya kupima saratani ya matiti katika hospitali ya Mloganzila  ni shilingi 3o,oo0 tu.

Akiongea na Watumishi wa  hospitali hiyo Makamu wa Rais amesema “Mnaofanya kazi sekta ya afya mnafanya kazi ya Uungu”

Makamu wa Rais pia aliwasikiliza wananchi waliofika kwenye kupata huduma hospitalini  hapo na kusema kuwa Serikali itajitahidi kushughulikia changamoto zinazojitokeza lakini aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya.

Mapema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy  Mwalimu alimuambia Makamu wa Rais kuwa (MAMC) Mloganzila ni kati  ya hospitali saba zinazomilikiwa na serikali ambazo zinatoa huduma za matibabu ya kibingwa ngazi ya juu pia alimpongeza Makamu wa Rais kwa kuweka msukumo wake katika huduma ya mama na mtoto ambapo juhudi  za Makamu wa Rais zimezaa matunda ambapo leo hii kuna  vituo 208 vimeboreshwa na kutoa huduma.

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi naTeknolojia Mhe. Ole Nasha amesema wanafunzi 350 wa shahada ya kwanza wameanza kupata mafunzo ya udaktari na udaktari bingwa na kuishukuru serikali  ya awamu  ya tano kwa kuona umuhimu wa maendeleo  ya upanuzi wa kamapsi hii ili  kuruhusu udahili wa wanafunzi wengi.

 

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *