Habari Kitaifa

Makamu wa Rais Awataka Viongozi wa Serikali Kukabiliana na Uharibifu wa Mazingira

on

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka  Viongozi wa ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati  na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais wa ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku  ya Mazingira  Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya  Mnazi mmoja.

“Nimuhimu, mipango ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu,” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kazi  ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi  ya mazingira  unahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote.

Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika India katika mji wa New Delhi ya kibeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafu ziwa mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati Mbadala”

Mapema leo, Makamu wa Rais alizindua ukuta wa bahari uliopo kwenye barabara ya Barack Obama wenye urefu wa mita 920, ukuta huo  ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi kavu unakadiriwa kuwa  na maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda na zipo faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na Tanzania kuwana Viwanda.

Mwisho, Makamu wa Rais amesema katika kufanikisha suala zima la uhifadhi waUtunzaji wa mazingira mi lazima tuifanye kila siku iwe siku yaMazingira.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *