Habari Kitaifa

Makatibu Wakuu 15 Kutafuta Suluhu ya Tishio la Kukauka Ziwa Manyara

on

Lango Kuu la Kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara ambapo Makatibu Wakuu zaidi ya 10 kutoka Wizara mbalimbali wametembelea kujionea hali ya tishio lililopo la Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akitoa neno la ukaribisho kwa Makatibu Wakuu  kutoka Wizara mbalimbali katika kikao cha Mawasilisho ya Taarifa ya Tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba.
Mwenyeji wa Ziara ya Makatibu Wakuu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akifanya Wasilisho la Taarifa kuhusu tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara,Maeneo ya Shoroba na Mitawanyiko ya Wanyama Tarangire -Manyara kwa Makatibu Wakuu hao.
Sehemu ya Ndege ambao ni kivutio kimojawapo kikubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ambao hutegemea pia uwepo wa Maji katika maeneo hayo ambayo kwa sasa yameanza kukauka kutokana na Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na Binadamu.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi (Mwenye kofia) akiwaonesha Makatibu Wakuu waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara maeneo ya Ziwa Manyara ambayo yameanza kukauka.
Eneo moja wapo la Vivutio vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara likionekana kuanza kukauka kutokana na Athari za kimazingira zinazosababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu zikiwemo ,Kilimo Uchimbaji wa Madini katika maene ya jirani na Ziwa hilo. 
Maeneo ambayo shughuli za Uchimbaji wa Madini umekuwa ukifanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Kijana akifanya shughuli ya uchekechaji wa Mchanga katika moja ya mito inayo peleka maji Ziwa Manyara ,shughuli hi imekuwa ikifanyika kwa lengo la kujipatia Madini ana ya Dhahabu ,Hata hivyo zoezi hili linatajwa kuwa moja ya Uharibifu wa Mazingira unaochangia kukauka kwa Ziwa Manyara.
 

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *