Habari Kitaifa

Makamu wa Rais akagua Mitaro ya Maji Jijini DSM

on

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye mpaka kati ya  Buguruni Mivinjeni na Sharifu Shamba pamoja na Mtoni kwa Azizi Ali kuwa watunzaji wazuri wa mitaro ya maji kwani ni mali yao wenyewe na si ya serikali.

Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kuta za bahari na mitaro ya maji jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi hao kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri shughuli za kiuchumi , kijamii na kimazingira.

Makamu wa Rais Makamu wa Rais alisema kila mmoja anapaswa kujishughulisha katika suala la kusafisha na kuhifadhi mazingira .

“ubaya wa mazingira ukiyaharibu yanakuadhibu” alisisitiza  Makamu wa Rais

Mtaro wa Buguruni Mivinjeni una urefu wa mita 475 na ule wa kwa Azizi Ali una urefu wa mita 550.

Makamu wa Rais alisema nchi inapozungumzia uchumi wa viwanda ni mazingira “tukiharibu mazingira hamna uchumi wa viwanda” hata viwanda vitakavyojengwa vinahitaji kutunza mazingira, visafishe maji yake kabla ya kutiririsha.

Makamu wa Rais alitoa rai kwa yeyote atakayebainika kuharibu miundo mbinu wanachukuliwa hatua za haraka.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kusema kuwa Usalama wa Nchi, Amani, afya, mazingira bora hayana chama hivyo ni jukumu la kila mmoja kuwajibika ili maendeleo yaweze kupatikana.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuongezeka kwa watu katika jiji la Dar es Salaam na mabadiliko ya tabia nchi kutaendelea kutoa changamoto za miundo mbinu hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kujenga miundo mbinu itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli zao kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *