Habari Kitaifa

MAMCU yasimamisha Minada ya Zao la Korosho Mtwara

on

Chama kikuu cha Ushirika Cha Masasi, Mtwara Cooperative Union (MAMCU) kimelazimika kusimamisha minada ya zao la Korosho iliyokuwa ikifanyika kila ijumaa kwa kipindi cha wiki mbili kutokana na wakulima kukusanya korosho ambazo hazijakauka hali inayoathiri Soko hilo.
 
Kaimu Meneja wa MAMCU Bw. Potency Rwiza anasema kupungua kwa mzigo katika maghala yanayosimamiwa na chama chake pamoja na kuwapo kwa Korosho ambazo hazijakauka kunaisababisha Korosho kushuka kilo na kupungua ubora mara inapouzwa kwa wanunuzi ambao wengi wao kutoka Nchi za nje.
 
Hata hivyo wakulima wa korosho wa mkoa wa Mtwara  wanafurahia kuuza korosho zao kwa shilingi elfu 4,055 kwa kilo bei ambayo ni kubwa ukilinganisha na minada iliyopita.
 
Mpaka kufikia sasa chama kikuu cha Ushirika cha MAMCU kimefika mnada wa tisa na tayari wameuza korosho tani elfu 84 na 97 zenye thamani ya shilingi bilioni 332.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *