Habari Kitaifa

Manispaa ya Kinondoni Yapitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha Mwaka 2018/2019

on

Baraza  la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni katika mkutano wake maalumu wa Baraza la Madiwani leo limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida  na mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019 ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajiwa kukusanya na kupokea kiasi cha Shilingi 242,185,292,987.00 ambapo shilingi 209,436,308,079.00 sawa na asilimia 86.5 ni ruzuku kutoka serikali kuu, shilingi 686,380,000.00  sawa na asilimia 0.3 ni mchango wa jamii na  shilingi 32,062,704,908.00 sawa na asilimia  13.2 ni mapato ya ndani ya manispaa.

Akizungumza mbele ya Madiwani wa Manispaa hiyo katika kikao hicho leo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta amesema kuwa kati ya fedha hizo zilizopitishwa, kiasi cha shilingi 120,326,705,873.00 ni matumizi ya kawaida ambayo ni sawa na asilimia 49.7 ya bajeti yote na  shilingi 121,858,587,114.00 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 50.3 ya bajeti.

Pia Meya Sitta ameeleza kuwa katika fedha hizo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi 32,749,084,908.00 kutoka vyanzo vyake vya ndani ambapo shilingi 16,392,166,400.00 zitatumika kwa matumizi ya kawaida na shilingi 16,356,913,508.00 zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo na  fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu ni shilingi 209,436,208,079.00 zitakazojumuisha kiasi shilingi 105,501,668,606.00 kwa  ajili ya miradi ya maendeleo.

Aidha mishahara ya watumishi kutokana na mapato ya ndani ni shilingi 906,498,855.00 na mishahara kutokana na ruzuku ya serikali kuu ni shilingi 99,590,270,811.00 na kufanya jumla ya shilingi 100,496,769,666.00 fedha kwa matumizi mengineyo ni shilingi 15,485,667,545.00 kutoka vyanzo vya ndani na shilingi 4,344,268,662.00 kutoka ruzuku ya Serikali kuu na kufanya jumla ya matumizi mengineyo kuwa ni shilingi 19,829,936,207.00.

Ili kufikia mafanikio yaliyokusudiwa Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni itaimarisha mahusiano mazuri kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wadau wengine itaendelea kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma  zilizo bora na za haraka, itaimarisha utawala bora uwajibikaji na uwazi na kujenga uwezo kwa viongozi wakiwemo waheshimiwa madiwani na  wenyeviti wa Serikali ya Mitaa  katika kusimamia  shughuli za wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Aidha mpango wa matumizi nabajeti ya mwaka 2018/2019 ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 hivyo matokeo ya utekelezaji wa  mpango na bajeti yameelekezwa katika kujibu matarajio ya watu ambayo ni utatuzi wa  kero zao pamoja na maisha bora kwa kila mtanzania.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *