Uchumi Zone

Maonyesho ya Bunge Property Expo Yatikisa Mjini Dodoma

on

Kampuni ya Terranova imeandaa maonyesho ya milki kuu, nyumba na nyenzo za ujenzi yanayofanyika katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Maonyesho hayo yaliyozinduliwa rasmi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi ambapo wadau mbalimbali walijitokeza kuonyesha bidhaa mbalimbali katika sekta hiyo wakiwemo, Nabaki Afrika, Fumba developments, Ngorongoro conservativation, Alrais developers na Taasisi ya Mwanamke Ardhi.
“Sisi tumeanza na tutazidi kuhamasisha wawekezaji wafike Dodoma , ili adhma kuu ya serikali ya kuhamia Makao makuu ya nchi izidi kupata tija kwa maendeleo yetu.” Alizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Terranova Bw. Emil Sylvester .
“Pamoja na ubunifu huo wa waandaji uliolenga kuwafikia watanzania wote kwa wakati mfupi kupitia wawakilishi wao, pia utasaidia kufikisha elimu kuhusiana na sekta nzima ya ardhi na kuiletea Tanzania mendeleo makubwa kutokana na rasilimali hii na naupongeza uongozi wa Kampuni ya kizalendo unaoongozwa na vijana waliopata  elimu katika vyuo vikuu vya  hapa nchini’ Alisema Mhe. Lukuvi.
Vilevile alitoa rai kwa wadau kulipa kodi halali katika uendeshaji wa shughili zao ili kwenda sawa na kasi ya ukuaji kiuchumi kupitia mapato ya ndani.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *