Habari Kitaifa

Mei Mwisho wa Uhakiki wa NGOs Nchini

on

Serikali imeagiza Mashirika yote yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha wanajihakiki katika Ofisi ya Msajili wa Mashirika hayo iliyopo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na ifikapo mwezi Mei mwaka huu na zoezi hilo litasitishwa rasmi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifunga kikao kazi cha wadau wa NGOs nchini kilichokuwa kinajadili kuhusu maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Bw. Katemba amesema kuwa zoezi hili limechukua muda mrefu sana na wamekuwa wakiongeza muda mara kwa mara ili kuyapa nafasi mashirika ambayo hayakujihakiki kufanya hivyo.

Ameongeza kuwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo mwezi Mei mwaka huu wataweka majina ya Mashirika yote ambayo yatakuwa yamejihakiki kwenye Tovuti mpya ya Msajili na yale yote ambayo yatakuwa hayajajihakiki hayataruhusiwa kufanya kazi nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bw. Nicholous Zakaria ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa NGOs kwa ushirkiano wanaowapa kama Baraza na kwa wadau wote wa NGOs nchini.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *