Habari Kitaifa

Mhandisi MAHENDA: PANGANI hydro Systems ipo Katika Hali Nzuri

on

Hali ya Upatikanaji umeme unaozalishwa kutokana na Chanzo cha Maji Kwenye Kituo cha Hale Mkoani Tanga, haitaathirika licha ya Mashine moja kati ya Mbili za Kufua Umeme kuwa katika mpango wa Matengenezo baada ya kuharibika Kwa Sababu ya Ukongwe.

Kabla ya Kupata hitilafu Mashine hiyo, Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale kilichoanza kazi Mwaka 1964 kilikuwa na uwezo wa Kuzalisha Megawati 21 za Umeme, ambapo Kutokana na Changamoto hiyo kwa sasa kimebaki Kufua Megawati 8 za Nishati hiyo.

Meneja Uzalishaji umeme wa nguvu ya Maji katika Kituo cha Pangani, Mhandisi Mahenda Stephen amedai hali hiyo haitaathiri Kwa Sababu vyanzo vya Kufua umeme Vimeongezeka huku akitolea mfano wa Vituo vya Pangani na Nyumba ya Mungu kilichopo Kilimanjaro.

Mhandisi MAHENDA akielezea Kituo cha Hale amesema Kihistoria Kituo hicho ni cha Kwanza Kufua umeme Chanzo kikiwa Maporomoko ya Maji baada ya Kujengwa mwaka 1961, ambapo Ukongwe wake ndio sababu ya Mashine moja ya Kuzalisha Nishati hiyo Kuharibika.

 Valvu ya kupitisha maji yanayopelekwa kwenye mashine za kufua umeme, kwenye kituo cha nguvu za umeme cha Hale ikivuja. Mhandsi Mahedna alielezea hali hiyo kuwa haina taathira kubwa na inatokana na mashine hizo kuwa na umri mrefu Zaidi.
 Bwawa la maji Pangani Pangani Falls.
 Mhandisi Mahenda akifafanua mambo mbalimbali ya kiufundi kwenye chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme cha New Pangani Falls.
 Exciter, moja kati ya mashine mbili ya kufua umeme kwenye kituo cha Hale, ambayo inafanya kazi. 
 Wahariri na wataalamu wa TANESCO, wakitembelea New Pangani Falls.
 Mhandisi Mkuu wa Pangani Hydro Systems, Lewis Loiloi, akitoa maeelzo kuhusu masuala ya kiusalama kwa wahariri wakiwa kwenye handaki, la New Pangani Falls.
Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha New Pangani Falls cha 132 kV.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *