Videos

Dkt MSONDE: Tutazifuta Shule Binafsi Iwapo Zitadanganya Mitihani ya Kidato cha 4

on

Baraza la Mitihani la Taifa NECTA limezitaka mamlaka zinazosimamia mitihani ya kidato cha nne mwaka 2017 ikiwemo shule binafsi, halmashauri na manispaa kujiepusha na udanganyifu ili kuifanya mitihani hiyo kuwa yenye tija kwa taifa.

Jumla ya watahiniwa 385,938 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2017 ili kupimwa uwezo na uelewa wao katika yale yote waliyojifunza kwa kipindi cha miaka minne.

Mtihani huu pia ni muhimu kwa taifa, wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla kwani matokeo yake huchagua wanafunzi watakaojiunga elimu ya juu ya Sekondari na kupata maarifa mbalimbali ya Afya, Kilimo, Ualimu na Ufundi.

Licha ya faida hizo baadhi ya wamiliki wa Shule binafsi hufanya udanganyifu katika matokeo hayo ili kuzinyanyua shule zao jambo ambalo linakemewa vikali na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania DK CHARLES MSONDE.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *