Habari Kitaifa

Moto wateketeza Soko la Mbagala Rangi Tatu, Jijini Dar es Salaam

on

Zaidi ya Wafanyabiashara 600 wa Soko la RANGI TATU lililopo MBAGARA jijini Dar es Salaam wamepata hasara baada ya Soko hilo kuteketea kwa Moto asubuhi ya leo.

Masaa kadhaa yaliyopita  eneo hili lilikuwa na Ofisi ya kudumu ya FATMA ambapo ilikuwa ni sehemu yake iliyomuingizia kipato vyerehani vyake ndio ulikuwa msingi wa Maisha yake.

Lakini sasa vyerehani vya FATMA vimegeuka kuwa chuma chakavu.

FATMA ni Mmoja wa Wafanyabiashara kati ya wafanyabiashara 600 waliokumbwa na janga la moto ulioteketeza soko lote la RANGI TATU lililopo Mbagala jijini DAR ES SALAAM asubuhi ya leo.

Ni Moshi tu ndio ulioshika hatamu katika eneo hili baadhi ya watu wanatumia fursa hiyo kujiokotea msalia ya vitu lakini baadhi ya wafanyabiashara wanakumbuka hasara waliyoipata.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *