Habari Kitaifa

Msajili NGOs Ataka Kusimamiwa kwa NGOs Ili Zifanye Kazi

on

Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGOs, Marcel Katemba amewataka Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzisimamia NGOs ili zifanye kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Wasajili Wasaidizi ili kutoka mafunzo kwa ajili ya kukumbashana majukumu yao Kama wasajili wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Amesema kuwa kimsingi Mashirika yasiyo ya Kiserikali bado hayatambui umuhimu wenu hivyo tutawakutanisha na Mashirika haya kwa ajili kufahamiana kiutendaji na kutambuana. 

Aidha Katemba amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakati mwingine yanakosa majibu muhimu kutoka kwa Wasajili Wasaidizi  hivyo kusababisha waone kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii sio watu sahihi kusimamia shughuli zao.

“Lengo la Mafunzo haya nikukumbashana mambo muhimu ambayo yatawafanya muweze kutoa majibu stahiki kwa Mashirika haya na kuyasimamia ipasavyo baada ya kujua shughuli wanazozifanya”alisisitiza Bw. Katemba.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya NGOs ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Baraka Leornard amewaambia wajumbe wa mafunzo haya kutoka Halmashauri zote kuzisimamia NGOs ili ziweze kuhudumia Wananchi. 

Bwana Baraka ameongeza kuwa kimsingi mafunzo haya ni ya kuwajengea uwezo wasajili wasaidizi wa serikali ili waweze kujua utaratibu wa kusajili na kuyasimamia Mashirika haya kwa matumizi mazuri ya fedha za umma wanazopata kupitia wafadhili wao.

“Pamoja na Masharika yasiyo ya Kiserikali kupata fedha kutoka kwa wafadhili ni muhimu wakatambua fedha hizo ni mali ya umma na ninyi wasajili wasaidizi mnayo haki yakujua matumizi ya fedha hizo,” alisisitiza Bw. Baraka. 

Mafunzo kama haya yamekuwa yanatolewa nchi nzima na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa  Wasajili Wasaidizi wa Mashirika haya ambao ni maafisa Maendeleo wa Jamii wa Halmashauri za Wilaya hapa Nchini.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *