Videos

MSAMA: Tutawashika Popote Maharamia wa Kazi za Wasanii

on

Kampuni ya Udalali ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imewatahadharisha wanaouza kazi feki za wasanii mbalimbali hapa nchini pamoja na waliowapangisha kuachana na kazi hiyo kwani ukamataji wa watu hao utaanza wakati wowote kuanzia sasa .

Sanaa ni sekta inayochukua nafasi kubwa sana katika maisha ya mwanadamu. Pia  imeweza kuajiri Watanzania wengi zaidi kuliko sekta nyingine nchini.

Lakini  wizi wa kazi za wasanii hao sio tu umekuwa ukiwanyonya wasanii, pia kuinyima Serikali mapato halali kwa ajili ya kuzitumia kwa maendeleo ya nchi.

Ambapo sasa kampuni ya Udalali ya Msama, imetangaza msako wa wezi wa kazi za sanaa kwa ujumla wake ambao wamekuwa kikwazo cha wahusika kutofaidi matunda ya kazi zao.

Operation hio itafanyika nchi nzima ambapo katika tathimini za awali mkoa wa mwanza pekee ndio umepunguza ufanyaji wa biashara hio.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *