Habari Kitaifa

MSD yaagizwa kuweka Nembo kwenye Dawa zinazonunuliwa na Serikali

on

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameiagiza Bohari ya Dawa (MSD) kuweka nembo za GOT dawa zote zinazonunuliwa na mfuko wa Serikali ili kuweka usimamizi mzuri na kuepusha uchepushwaji wa dawa hizo katika maduka ya dawa binafsi.

Waziri Ummy amesema hayo wakati akiendelea na ziara ya kukagua hospitali za mikoa ambapo leo ametembelea hospitali ya Amana iliyopo jijini Dar es salaam, na kukuta changamoto mbalimbali ikiwemo msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo na kuagiza uongozi wa hospitali kushughulikia changamoto mbalimbali  za wagonjwa  zinazowakuta ikiwemo wingi wa wagonjwa.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *