Viwanjani

Mwakyembe: Viongozi Tambueni na Kuyalinda Maeneo Yaliyotumika katika harakati za Urithi

on

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (kulia) akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) alipotembelea Mkoani Morogoro Jana kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati wa ukombozi wa Bara la Afrika. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhe. Clifford Tandari.

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Dakawa Bw. Beatus Nyakunga (kulia) akimwonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye miwani) ramani ya mazingira ya Dakawa yaliyotumika wakati wa harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika alipotembelea Mkoani Morogoro Jana kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Dakawa Bw. Dornald Gwilaje (kushoto) akimpa  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) taarifa ya eneo la Dakawa lililotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika alipotembelea Mkoani Morogoro Jana kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.

Mkuu wa Chuo cha VETA Dakawa Bw. Beatus Nyakunga (wapili kulia) akimwelezea Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) mafanikio ya chuo hicho tokea kipindi cha harakati za ukombozi wa bara la Afrika alipotembelea eneo hilo jana Mkoani Morogoro kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika. Wapili kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhe. Clifford Tandari.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaomba viongozi wa Mkoa wa Morogoro kushirikiana na wananchi wa mkoa huo kutambua na kulinda maeneo yote yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika kwani huu ni wajibu na heshima tuliyopewa na bara la afrika kuwa makao makuu ya kuhifadhi historia hiyo.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jana mkoani Morogoro alipotembelea maeneo mbalimbali yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa bara la afrika na kuahidi kuyalinda maeneo hayo kwa vizazi vijavyo ili historia hiyo nzuri ya nchi yetu katika kukomboa nchi nyingine za afrika irithishwe kwa vizazi vijavyo.

“Wizara imeamua kupita katika mikoa yote yenye kumbukumbu ya ukombozi wa bara la afrika kuangalia maeneo hayo na kuhakikisha maeneo hayo yanalindwa kwa ajili ya kizazi cha leo cha kesho na hata cha kesho kutwa” amesema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Tanzania  imepewa jukumu kubwa na umoja wa afrika mnamo  mwaka 2011 na viongozi wakuu wa umoja wa afrika kwa kuiteua Tanzania kuwa makao makuu ya kuhifadhi historia ya ukombozi wa bara la afrika na kuteua jiji la Dar es Salaam kuwa ndipo patakapojengwa Ofisi za kumbukumbu ya Ukombozi wa Bara la Afrika.

“Hii ni fursa ya pekee kwa Tanzania kwa miaka ijayo kuwa na chombo kikubwa cha kuvutia utalii wa kiutamaduni kwa nchi za Afrika kwani itawezesha kupanua wigo wa utalii ndani ya Tanzania kupitia maeneo yaliyotumika wakati wa ukombozi lakini pia kupitia makaburi yaliyohifadhi miili ya waafrika wenzetu waliofariki hapa nchini wakati wa harakati hizo” aliongeza Dkt. Mwakyembe.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema kuwa Program ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika katika mkoa wa Morogoro ni muhimu kwani itasaidia kuubeba mkoa huo katika masuala ya utalii kutokana na mkoa huo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika harakati za ukombozi wa bara la afrika,

Aidha Dkt. Kebwe ameiomba Wizara yenye dhamana na harakati za ukombozi wa bara  la Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu kutoa ushirikiano kwa taasisi zilizojengwa na wanaharakati hao kuinua maendeleo ya Mkoa wa Morogoro pamoja na utalii wa utamaduni ndani ya nchi yetu.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *