Habari Kitaifa

Mwanahabari Nguli Muhingo Rweyemamu azikwa Makaburi ya Kinondoni

on

Mwili wa Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga na Mwandishi Nguli nchini MUHINGO RWEYEMAMU umeagwa hii leo na kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Nyuso za huzuni, wapo ambao tayari mioyo yao imeafiki lakini kwa wengine bado imekuwa na ugumu kuafiki.

Ukweli ni kuwa hatunae tena nguli huyu wa tasnia ya habari nchini marehemu MUHINGO RWEYEMAMU.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo DK HARRISON MWAKYEMBE ameongoza shughuli za kuaga mwili wa Nguli huyo kabla ya kwenda kumpumzisha katika nyumba yake ya milele.

Nenda MUHINGO, nenda Nguli wa tasnia ya habari, utakumbukwa daima.

Watoto wa Marehemu, Muhingo Rweyemamu ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Wakuu wa Wilaya Wastaafu, wakiweka Shada la Ua juu ya Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu wakati wa maziko katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu (wa pili kushoto), akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani (TASWA), Juma Pinto wakati wa shughuli ya kumuaga mwanahabari mkongwe,marehemu  Muhingo Rweyemamu, Kulia ni Benny Kisaka na kushoto ni Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula.
Sehemu ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili wa  marehemu Rweyemamu.
Wanahabari wakirekodi tukio hilo.
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Mtanzania, ambaye pia alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Muhingo, akitoa salamu za rambirambi.
 Mtoto wa marehemu Muhingo, Emmanuel  akisoma wasifu wa marehemu baba yake.
Wajumbe wa kamati ya mazishi ya marehemu, Muhingo, wakijadiliana jambo wakati wa kuuaga mwili. Kutoka kushoto ni Joyce Mmasi, Mgaya Kingoba, Theiphil Makunga, Abubakar Liongo na Benjamin Thomson.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk, Harrison Mwakyembe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhingo kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhingo.
 Sophia Mjema akimfariji mjane wa Marehemu Muhingo, Bi Roseline.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akimfariji mjane wa marehemu Muhingo, Rweyemamu.
Waombolezaji wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhingo.
Mpiga picha wa zamani wa Daily News, Athuman Khamisi akimfariji mjane wa marehemu, Roseline.
Mama mkwe wa marehemu, Muhingo, akilia baada ya kutoa heshima za mwisho.
Roseline Rweyemamu (katikati) ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, akiugusa mwili wa mumewe wakati wa kuaga.
Waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu baada ya kuutolea heshima za mwisho kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *