Videos

MWIGULU : Dereva wa Tundu Lissu ni Shahidi Muhimu kwenye Upelelezi Wetu

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Usalama wanaendelea kuchunguza tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Mh. Tundu Lissu lililotokea Septemba 7 mwaka huu huko nyumbani kwake Area D, Dodoma.

Akizungumza katika kituo cha Televisheni cha Clouds 360 asubuhi leo, Waziri Nchemba amesema kuwa walitamani Dereva wa Lissu ahojiwe mapema ndio maana Polisi Dodoma walitoa wito afike kuhojiwa lakini ziko taarifa kuwa Dereva huyo anapatiwa matibabu Nairobi Kenya.

Hata hivyo Waziri Mwigulu amesisitiza kuwa Dereva huyo anasubiriwa akimaliza matibabu ili ahojiwe na Polisi.

Aidha, Waziri Nchemba amesema kuwa, kufuatia tukio hilo tayari magari 10 yanayofanana na lililohusika na shambulio la Lissu yamekamatwa kwa upelelezi.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *