Habari Kitaifa

OIF Yaeleza Fursa Zilizopo kwa Watanzania Wanaojua Kifaransa

on

Shirika la Kimataifa la La Francophonioe (OIF) ambalo linajumuisha nchi 84 ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa limesema kwamba ni muhimu kwa Watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa kwa sababu kuna fursa nyingi wanaweza kuzipata kwa kuzungumza lugha hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier amesema katika nchi hizo kuna nafasi za kazi nyingi ambazo kama Watanzania watajifunza Kifaransa wanaweza kuzipata.

Alisema Tanzania inazungukwa na nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa kama Burundi, Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na hivyo kwa wananchi wa Tanzania hiyo ni fursa ambayo wanaweza kuitumia katika shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier akizungumza kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25.

“Hapa Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu waitumie.”

“Tanzania inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza Kifaransa,” alisema Clavier.

Aidha, Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française, Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *