Habari Kitaifa

Polisi TAZARA Watoa onyo kwa Wahalifu mafuta katika Shirika hilo

on

Jeshi la Polisi nchini limewaonya badhi ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)  ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta na miundombinu mbalimbali ya shirika hilo kuacha mara moja.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi Mwandamizi Patrick Byatao wakati wa hafla fupi ya kuwatunukia zawadi baadhi ya Askari waliofanya vizuri katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya shirika hilo ambapo baadhi yao walifanikiwa kuwakamata watumishi wa shirika hilo wakiiba mafuta.

“Katika siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watumishi wa shirika hilo wasio waaminifu ambapo wamekuwa wakilitia hasara shirika hilo jambo ambalo tunanaendelea kuimarisha usalama ili kuhakikisha kuwa tunawadhibiti, na kikosi chetu kitaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha tunakomesha tabia hiyo ambayo imekuwa ikidhoofisha utendaji wa TAZARA pamoja na kuitia hasara Serikali” alisema Kamanda Byatao.

Akizungumzia utoaji wa zawadi hizo Kamanda Byatao amesema askari hao kumi wamefanya vizuri kwa kujituma katika kipindi cha mwaka 2017 hivyo kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi ni vyema kuwazawadia ili kuongeza morali yao ya kazi na kuwafanya wengine kuendelea kujituma zaidi.

Kwa upande wake mmoja wa Askari waliopata zawadi baada ya kufanya vizuri WP Nina Dachi amewaasa askari wenzanke kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuhakikisha kuwa miundominu ya shirika hilo inakuwa salama wakati wote.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *