Habari Kitaifa

Polisi yataja Sababu za Kumwachia Mwanasiasa Hashim Rungwe

on

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemwachia kwa dhamana, Mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA, Hashim Rungwe.

Mwenyekiti huyo wa CHAUMMA aliingia matatani Baada ya akituhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Tayari RUNGWE ambaye pia ni Mwanasheria ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa takribani siku nne.

Kwa mujibu wa Kamishna huyo wa Kanda Maalum ya Dar es salaam LAZARO MAMBOSASA,  Hashim Rungwe akiwa Wakili anatuhumiwa kushiriki kufanya udanganyifu kwa Mfanyabiashara kutoka Uturuki ambae alikuja nchini kununua korosho tani 15.

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *