Habari Kitaifa

Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuijengea Heshima Taifa

on

Serikali yatao Milioni Mia saba kwa ajili ya ukarabati wa Jengo lilokuwa Makao Makuu ya Wanakamati wanaopigania Uhuru wa kulikomboa Bara la Afrika ikiwa ni sehemu ya kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alipotembelea ofisi zinazoratibu programu hiyo ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika leo jijini Dar es Salaam kupata taarifa ya maendeleo ya programu hiyo.

‘’Tumepewa dhamana na heshima kubwa na Umoja wa Afrika ya kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika sababu ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere alivyopigania uhuru wa bara la afrika na kutoa ofisi jijini Dar es Salaam ambayo ilikuwa Makao Makuu ya wapigania Uhuru kutoka nchi mbalimbali za Afrika kukutania na kupanga mikakati hivyo ni vyema tuhifadhi historia hii,’’ Dkt. Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika ziara yake ofisini hapo Waziri Mwakyembe alisema serikali inampango wa kujenga ofisi kubwa na za kisasa katika maeneo ya Bunju Mwabepande jijini Dar es Salaam ambazo itahifadhi historia yote na hapo patakuwa ni kituo cha Kimataifa ambacho watalii na wageni mbalimbali watatembelea na kupewa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.

Kwa upande wa Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi Ingiedi Mduma alieleza kuwa kituo hicho kitakachojengwa kitakuwa ni moja kivutio cha utalii na kitasaidia kuiingizia serikali mapato  kutoka na wageni watakao kuwa wakitembelea kituo hicho na eneo lake linakaribia ekari hamsini.

Pamoja na haya Mheshimiwa Mwakyembe alitoa wito kwa watanzania kuhifadhi na kutunza maeneo yaliyotumika na mashujaa hao waliyokuwa wakipigana kukomboa bara la Afrika pamoja na kutoa taarifa za maeneo wanayojua yalitumika na mashujaa hawa kwa lengo ya kuisaidia serikali ili iweze kuhifadhi historia hiyo adhimu yenye kulipa Taifa heshima kubwa.

Hata hivyo serikali imeanda muswada utakao pelekwa bungeni kwa ajili ya kupatikana kwa sheria itakayosimamia vyema historia mbalimbali za taifa letu.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *