Habari Kimataifa

Raila Odinga: Safari ya Canaan Haiwezi Kuzuiwa

on

Mgombea urais wa upinzani Raila Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika.

Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais.

Imetoa mfano mwema.

“Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa, Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan.”

Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.

Wakili mkuu wa Bw Odinga, James Orengo, amesema mahakama imefuata katiba kubatilisha uchaguzi wa urais.

Amesema anatumai tume itaandaa uchaguzi wa marudio kwa njia huru na ya haki.

“Desturi ya kutoheshimu sheria lazima ikomeshwe na wahusika waadhibiwe. Mwaka 2013, maafisa wa tume ilibainika kwamba walifanya makosa. Tume imo mashtakani. Kabla tufanye uchaguzi mwingine, tume lazima ichunguzwe.

Sidhani tutakuwa na tume hiyo ikiandaa uchaguzi tena.”

Jaji Mkuu David Maraga ameagiza: Uuchaguzi wa urais uliofanyika 8 Agosti, 2017, haukuandaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo matokeo yake ni batili.

“Natangaza hapa kwamba Bw Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa.

“Agizo linatolewa, kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha uchaguzi mwingine kwa kufuata katiba na sheria katika kipindi cha siku 60.”

About Habari360_1

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *