Habari Kitaifa

Rais JPM Mgeni Rasmi Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Iringa

on

Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambao ni waandaaji wa sherehe za wafanyakazi kitaifa (MEI  MOSI) wamempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kukubali mwaliko wao wa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mei Mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa.

Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Vyamhokya alisema leo kuwa katika sherehe hizo za wafanyakazi duniani kwa Tanzania zitafanyika katika mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa Samora na kuwa tayari Rais Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi.

Hivyo aliwataka wafanyakazi kujitokeza kwa wingi kushiriki sherehe hizo na kuwa kupitia sherehe hizo watapata fursa ya kujua mikakati ya serikali dhidi ya wafanyakazi nchini japo hadi sasa wanapongeza hatua iliyofikiwa na serikali ya kuwarejesha kazini wafanyakazi waliokuwa wamesimamishwa kazi kutokana na elimu yao ya darasa la saba.

Rais  huyo alisema kuwa TUCTA imefanya jitihada kubwa za kukutana na serikali kuwapigania wafanyakazi hao walioondolewa kazini  kutokana na  elimu yao na serikali imesikiliza na imewarejesha kazini.

Alisema kuwa serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa kuongeza ajira pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wafanyakazi na kuzipatia majibu.

Akielezea juu ya maandalizi ya sherehe za mei mosi mkoani Iringa alisema kwa sehemu kubwa maandalizi yanakwenda vizuri na wamepata ratiba ya kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Iringa kutoa elimu pamoja na kukututana na wafanyakazi ili kujua changamoto zao.

 ” TUCTA inapenda kuishukuru serikali ya mkoa wa Iringa kwa kukubali kupokea maadhimisho haya ya Mei mosi 2018 TUCTA kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Iringa chini ya Mkuu wa Mkoa, Amina Masenza pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama tumefanya maandalizi ya kutosha” Alisema Rais wa TUCTA.

Aidha amesema kabla ya Mei mosi mambo yakayofanyika Iringa ni pamoja na makongamano mawili ya Kimkoa na moja la kitaifa na kuwa kongamano la kwanza litafanyika April 23 katika wilaya ya Mufindi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jamhuri Wiliam wakati  kongamano la pili litafanyika wilaya ya Kilolo April 25  na mgeni rasmi ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah huku April 27 litafanyika kongamano la kitaifa litakalohusu Tanzania ya uchumi wa viwanda kwenye ukumbi wa Kichangani ambalo viongozi mbalimbali  wa kitaifa watashiriki.

Aidha alisema kutakuwa na michezo ya Mei mosi ya fani mbalimbali itakayoanza April 16 hadi 30 katika uwanja wa Samora kuwa kwa ajili ya kuwafanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia fursa ya mei mosi Iringa maonyesho ya bidhaa mbali mbali yatafanyika.

 

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *