Habari Kitaifa

RC MAKONDA Afanya Ziara na Kukagua Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya BAKWATA

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA ambapo amefurahishwa na kasi ya ujenzi huo.

Akizungumza wakati alipoenda kutembelea ujenzi huo unaoendelea Mhe. Makonda amesema kazi wanayofanya Viongozi wa Dini ni kubwa hivyo wanapaswa kuthaminiwa kwa kuwaweka katika mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Ujenzi wa jengo hilo la kisasa unaofanywa na jitihada za Mhe. Makonda kuthamini na kuwapa heshima Viongozi wa Dini kwa kuhakikisha wanafanyakazi katika mazingira mazuri na yenye hadhi kutokana na thamani na mchango wao mkubwa katika jamii.

Aidha Mhe. Makonda ameongeza kuwa shauku yake ni kuona hadi kufikia mwezi wa Ramadhani jengo linakuwa limekamilika na kuanza kutumika, na kuwaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Amani Taifa la Tanzania na viongozi wake.

Kwa upande wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi amemshukuru Makonda kwa kuwajengea jengo hilo na kusema katika miaka 50 BAKWATA haijawahi kuwa na jengo zuri na la kisasa kama hilo hivyo Mhe. Makonda anaweka historia ya kwanza.

Mufti Zuberi amesema kuwa jengo lililokuwepo lilikuwa likiwafanya kuona hata aibu hata kupokea ugeni wa viongozi wa kislamu ulimwenguni.

Katika ziara hiyo Viongizi wa Dini kwa pamoja walimuombea Dua Mhe. Makonda pamoja na *Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwezesha kujengwa kwa Msikiti wa Mfalme wa Morocco wenye uwezo wa kuchukuwa watu 8,000 ambapo ujenzi bado unaendelea.

Jengo hilo la kisasa lenye Ghorofa Nne pamoja na Ground floor lina Ofisi ya Mufti wa Tanzania, Ofisi ya Katibu, VIP room, kumbi za mikutano, ofisi za wafanyakazi, ofisi za mshauri, Jiko, Vyoo, sehemu ya Kufanya Dua pamoja na sehemu ya mapokezi. 

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *