Habari Kitaifa

RC Makonda akabidhi Kadi za Bima ya Afya (Toto Afya Kadi)

on

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amekabidhi kadi 220 za Bima ya Afya (Toto Afya Kadi) zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11 kwa watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wapate uhakika kwa matibabu ya mwaka mzima.

Makonda amesema kuwa kawaida Mwezi Mtukufu watu wamekuwa wakifuturisha watoto yatima lakini inakuwa ni chakula cha siku moja kwa hiyo katika mwenendo wa mwezi mtukufu ameona ni vyema aguse maisha ya watoto yatima kwa kuwapatia Bima ya Afya ambapo ameamua kuanza na watoto 220 na baadae kuongeza wengine.

Aidha Makonda amesema kadi hizo zitawawezesha watoto kupatiwa matibabu bure kwa kipindi cha mwaka mmoja katika hospitali yoyote hapa nchini.

Hata hivyo Makonda amesema watoto waliopatiwa kadi hizo hawahusiani na wale waliojotokeza kwenye zoezi la kutafuta haki ya mtoto ambapo ameishukuru hospitali ya Regency na  TMJ  kwa kujitolea kutoa kadi hizo.

Sambamba na hilo Makonda amesema atakabidhi pia mabegi 400 yaliyosheheni vifaa vyote vya shule kwa vituo vya watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wawe na uhakika kwa kupata masomo mwaka mzima na kuweza kutumia vyema fursa ya elimu bure.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Regency Dkt. Kanabar Rajni na Mkurugenzi wa hospitali ya TMJ Bi. Parul Chhaya kwa pamoja wamesema wameguswa kutoa msaaada huo kama sehemu ya kuunga hamasa anayoitoa Makonda kwa wazazi kuwa na kadi za bima za afya.

About Habari360_TZA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *